Meneja
wa benki ya Exim Tanzania tawi la Mbeya, Bw Iddy Mwacha(kushoto)
akikabidhi msaada wa vitabu vya masomo kwa mmoja wa wanafunzi
aliewawakilisha wanafunzi wenzie na uongozi wa shule ya sekondari Sinde
iliyopo eneo la Mwanjelwa mkoani Mbeya katika kupokea msaada huo ikiwa
ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika kuisadia serikali
kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa nchini. Wanaoshuhudia
ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, uongozi wa shule pamoja na
wanafunzi.
BENKI
ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitabu vya masomo vyenye thamani ya
sh mil. 8/- kwa shule ya sekondari Sinde iliyopo eneo la Mwanjelwa
mkoani Mbeya ikiwa ni mwendelezo wa harakati za benki hiyo katika
kuisadia serikali kuboresha hali elimu na ufaulu wa wanafunzi hapa
nchini.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu hivyo iliyofanyika kwenye
viunga vya shule hiyo mwishoni mwa juma lililopita, Meneja wa benki hiyo
tawi la Mbeya Bw Iddy Mwacha alisema msaada huo ni sehemu ya
uthibitisho wa namna benki hiyo imekuwa ikipambana kuhakikisha uwepo
wake hapa nchini unaleta tija zaidi kwa jamii.
Alisema
kipaumbele kwenye elimu ni muhimu kutokana na ukweli kwamba sekta
mbalimbali ikemo ile benki ili zifanye vizuri zaidi zinategemea uwepo wa
wasomi kuziendesha na jamii iliyoelimika kwa ujumla.
“Ni
kutoka na kufahamu ukweli huo ndio maana siku zote tumekuwa
tukihakikisha kwamba kile tunachokipata tunagawana na jamii ikiwemo
kuboresha ubora wa elimu ili mwisho wa siku tupate matokeo mazuri
kielimu,’’ alibainisha.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mkuu wa shule hiyo Mwl Shadrack Mwakasyama licha ya
kuishukuru benki ya Exim kwa msaada ilioutoa, pia aliwahikikishia
viongozi wa benki hiyo kuwa yeye na walimu wote wa shule hiyo watakuwa
mstari wa mbele katika kuhakikisha vitabu hivyo vinatumiwa ipasavyo na
umakini mkubwa.
“Shule
yetu kiukweli bado inakabiliwa na changamoto kadhaa na ndio sababu
tunawahikikishieni kwamba tutajitahidi kuhakikisha kwamba kila msaada
unaolenga kupunguza changamoto hizi tunauenzi kwa nguvu zetu
zote…asanteni sana!,’’ alipongeza.
Aliongeza
kuwa ongezeko la vitabu shuleni hapo litakuwa kama chachu ya kutimia
kwa malengo ya serikali katika kuhakikisha kwamba ubora wa elimu hapa
nchini unakuwa kwa kuridhisha.
Aidha
Mwl Mwakasyama alitoa wito kwa mashirika na taasisi nyingine kuiga
mfano huo huku akiongeza kuwa kwa sasa serikali peke yake haiwezi
kutatua changamoto zote zinazoikabili sekta ya elimu hivyo nguvu ya
wadau mbalimbali ni muhimu.