MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 15, 2015

P-SQUARE WAONYA: SISI WABURUDISHAJI SI WANENGUAJI

Mapacha wa muziki wa R&B wa Nigeria, Peter na Paul Okoye.
MAPACHA wa muziki wa R&B wa Nigeria, Peter na Paul Okoye wanaounda kundi la P-Square, wamesema hawataki kuitwa wanenguaji, bali waitwe waburudishaji.

Wasanii hao ambao hivi sasa wanachukuliwa kuwa waimbaji bora zaidi barani Afrika, wamesema wanajisikia vibaya kuitwa wanenguaji, kwani kuna mambo mengi wanayoyafanya katika tasnia ya muziki.“Nimezoea kuwasikia watu wakisema nawapenda P-Square kwani wanajua kucheza, lakini ukweli ni kwamba huwa sipendi watu watuite wanenguaji.
“Ni vyema wakatuelezea kuwa sisi ni waburudishaji na wanamuziki kwani hivyo ni vizuri zaidi,” alisema Peter na kuongeza kwamba nyimbo za mapenzi hivi sasa hazina masoko sana nchini Nigeria kama baadhi ya mashabiki wanavyodai, akisema nyimbo za mapenzi ambazo ziliwahi kuwika sana ni ‘Olufunmi’ wa Styl Plus na ‘Beautiful Onyiye’ wa P-Square.
“Hivi sasa nyimbo za mapenzi hazina soko kwani ni za kizazi kingine. Hata hivyo, kwa vile bado kuna mashabiki kadhaa wanazipenda, tutazifufua, alimalizia akijibu hoja ya shabiki mmoja aliyemwambia anapenda kuzisikiliza nyimbo zao za mapenzi.