Rais wa Burkina Faso Michael Kafondo amenyang’anywa madaraka ya kuendelea kuiongoza nchi hiyo baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa Taifa hilo Blaise Compaore.
Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi hao wawili wa Serikali Kafondo pamoja na Waziri Mkuu wake Isaac Zida kuzuiliwa kuingia kwenye mkutano wa Mawaziri na walinzi waliokuwa wa Rais Compare.
Vurugu zilitanda katika mji mkuu wa
nchini hiyo Ouagadougou huku risasi zikirushwa hovyo hewani ili
kuwatawanya waandamanaji waliojitokeza kwa wingi kupinga rais huyo
kuendelea kubaki madarakani.
Shirika la Voice of America
limesema Rais huyo, Waziri mkuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali
waliwekwa chini ya ulinzi na kikosi cha usalama RSP kinachomsapoti Rais
aliyeondoka madarakani Blaise Compaore.
Compaore aliondolewa madarakani kwa
nguvu ya wananchi Octoba 2014 na kuteuliwa Rais wa mpito kabla ya
kufanyika kwa uchaguzi mkuu October 11 mwaka huu