MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 17, 2015

Najipanga kwenda kutafuta Modeling Agency nje, za hapa Bongo hazilipi – Miss Universe TZ 2014

miss universe
Caroline Benard (katikati)
Miss Universe Tanzania 2014, Caroline Benard amesema kuwa kwa sasa anajipanga kwenda kutafuta Modeling Agency za nje ya nchi baada ya kugundua za hapa Bongo zimeshindwa kumtimizia ndoto zake.“Najipanga kwenda kutafuta Modelling Agency za nje coz za hapa Bongo hazilipi. Nipo kwenye modeling toka 2013 hadi leo but still hadi leo sijafika pale ninapotaka.” Caroline aliliambia jarida la Baabkubwa.
Ameongeza kuwa moja ya ndoto zake ni kuja kuwa Super Model wa Afrika, ndio sababu yuko kwenye mipango ya kutafuta Agency kubwa zaidi nje ya nchi kama vile Ice Models na Boss za Afrika Kusini.