Mwana FA anaweza kuwa busy akizunguka kwenye kampeni lakini anatumia muda huu pia kurekodi ngoma mpya.Ngoma ya mwisho ya FA ilikuwa ni ile aliyomshirikisha Alikiba, Kiboko Yangu iliyompa tuzo ya KTMA 2015.
FA amepost picha akiwa studio na P-Funk Majani hali inayoashiria kuwa ngoma ijayo itatoka Bongo Records.
“So guess what…..? cc @majani187,” aliandika FA kwenye picha hiyo.