Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,
Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Jimbo la Bumbuli mkoani
Tanga jana wakati wa mkutano wa kampeni za CCM.
Sehemu ya umati wa wananchi ulifurika kwenye mkutano huo wa kampeni katika Jimbo la Bumbuli
Mtoto akiimba kwa ufasaha wimbo wa kuhimiza watu kwenda kupiga
kura Oktoba 25, mwaka huu na kumpigia kura Dk Magufuli ili ashinde
urais.
Dk Magufuli akiwa amembeba mtoto huyo baada ya kufurahishwa na
uimbaji wake katika mkutano wa kampeni Kata ya Malamba, Wilaya ya
Nkinga.
Mmoja wa wazee wa Kata ya Malamba akiwa na furaha baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli.
Msanii Joti wa kikundi cha uchekeshaji cha The The Orijino Komedi akimchukua Dk Magufuli ili ajumuike nao kucheza muziki wakati wa kampeni hizo.
Dk Magufuli akijumika kucheza muziki na wasanii wa kikundi cha The Orijino Komedi
Baadhi ya wazee wa Kata ya Malamba, mkoani Tanga, wakiwa na picha za Dk Magufuli
Dk Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Nkinga
Baadhi ya vijana wakishangilia baada Dk, Magufuli kutoa ahadi
kuwa akishinda Serikali yake itakuwa inatoa kwa kila kijiji sh. mil 50
kwa wazee na vijana kwa ajili ya mikopo ya kuanzishia miradi ili
wajikimu kimaisha.
Wananchi wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya Dk Magufuli katika Kijiji cha Mashewa
Dk Magufuli akimnadi Mgombea ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani 'Prof Maji Marefu"
Akimpunia mkono mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk Magufuli.
Mfuasi wa CCM akishangilia kwa furaha baada Mgombea urais, Dk
Magufuli kuahidi kwamba akishinda wataanzisha utaratibu wa
kuwakopesha wanawake na Vijana kwa kila kijiji kupatiwa shmil 50.
Mkutano huo wa kampeni umefanyika katiuka Kata ya Matalawanda.
Dk Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi, mgombea ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani
Wafuasi wa CCM wakiwa wameshikilia bango hilo katika mkutano wa kampeni mjini Korogwe
Dk magufuli akijinadi kwa wananchi katika mji wa Mombo
Katibu Mkuu msitaafu, Yusufu Makamba akielezea sifa lukuki
alizonazo Dk Magufuli tofauti na mgombea kupitia Umoja wa Katiba ya
wananchi
Dk Magufuli akiteta jambo na January Makamba
Wasani wa The Orijino Komedi wakilishambulia jukwa wakati wa mkutano huo
Mwakilishi wa watu wenye ulemavu Amon Mpanju akielezea jinsi
CCM inavyo wajali watu wa namba hiyo wakati wa mkutano mjini Lushoto
jana
Dk Magufuli akimtambulisha kwa wananchi Mgombea ubunge Jimbo la Bumbuli, January Makamba
Wagombea udiwani Jimbo la Bumbuli wakitambuliwa kwa wananchi katika kkiutano huo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu akimnanga Frederick Sumaye kwa ni fisadi zaidi ya Lowassa.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mlalo, Hassan Ngwilizi akimpigia chapuo Dk Magufuli katika mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya kaampeni ya CCM, Ummy Mwalimu akimpigia debe Dk Magufuli wakati wa mkutano huo
Dk Magufuli akijinadi mjini Lushoto.
Akishinda urais Dk Magufuli amehidi kujenga barabara ya
lami kutoka Soni hadi Bumbuli yenye umbali kwa Km 22. Pia ameahidhi
kuharakisha mchakato wa kukikabidhi kiwanda cha chai cha Mponde kwa
wananchi na kuanza kuzalisha.
Pia ameahidi kuboresha hali za wanajeshi, walimu na wafanyakazi nchini
Dk Magufuli ambaye kampeni zake huzifanya kwa magar, tayari hadi sasa
kafanya katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara,
Morogoro na Tanga na leo anaanza kampeni katika Mkoa wa Mara.