Amber Rose atoka na Mwanamichezo Odell Beckham Jr.
Mwanamichezo Odell Beckham Jr 
New York, Marekani
INAONEKANA mwanamitindo nyota wa
Marekani, Amber Rose (31), ameachana moja kwa moja na mumewe, Wiz
Khalifa, kwani inasemekana mrembo huyo ameanza uhusiano wa kimapenzi na
mchezaji wa timu ya New York Giants, Odell Beckham Jr. (22).
Vyanzo mbalimbali vinasema, mwanariadha
huyo amekuwa akimfuatilia mrembo huyo kwa miezi kadhaa kabla ya kumpata
kupitia rafiki yake na hatimaye kutoka naye katika matukio kadhaa, ikiwa
ni pamoja na kuonekana ‘wakila bata’ kwenye mgahawa wa TAO jijini New
York mwezi uliopita.
Pia habari zimesema Odell alimshangaza
Amber kwa kumpa kitita cha maua ambayo ni alama ya upendo. Hii ni mbali
na kuonyesha upendo wake kwa Amber katika mtandao wa Twitter
alipoandika maneno kuhusu penzi la hilo.
Amber alianza kutoka na rapa, Wiz,
mapema mwaka 2011 kabla hawajachumbiana mnamo Machi 2012 na baadaye
kufunga ndoa mwaka uliofuata na kumpata mtoto wa kiume aitwaye Sebastian
Taylor, Februari
21, 2013.
Septemba 2014 Amber alifungua kesi kuomba talaka dhidi ya rapa huyo akidai ni kutokana na mambo ambayo hayawezi kusuluhishwa.