Dar es Salaam, Tanzania
Kampuni ya mawasiliano ya Airtel
Tanzania imeendelea kuwafanya wateja wake mamilionea kupitia promosheni
yake ya “Jiongeze na Mshiko”. Habibu Mwella Freuzi, mfanyabiashara
kutoka Dar Es Salaam na Kitabu Ally, mkulima anayeishi Kigoma
wamepatikana kuwa washindi wa million moja na million tatu baada ya droo
ya kuchezesha droo ya nane katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini
Dar Es Salaam.
Afisa Uhusiano na Matukio, Dangio Kaniki, alisema kuwa bado kuna
zawadi nyingi kushindaniwa kati ya sasa mpaka Novemba atakapopatikana
mshindi wa mwisho wa droo hii, atakayeondoka na kitita cha shililingi
milioni 50. Hivyo aliwahimiza watanzania kuchukua fursa hii waliopatiwa
na Airtel kujiinua kiuchumi.
Hadi sasa, promosheni ya “Jiongeze na
Mshiko” ya Airtel imewafanya watanzania 16 mamilionea. Mamilionea zaidi
wanategemewa kutokea katika promosheni hii iliyoanzishwa wiki saba
zilizopita. Vile vile Airtel imewazawadia fedha taslimu washidi wa droo
ya saba, ambao ni, Geri William kutoka Dar es Salaam na Lui Saulo
Karunda, mkazi wa Kigoma.
Wateja wanaweza kujinga na promosheni
hii bure kwa kutuma ujumbe wenye neno "BURE" kwenda namba 15470, na
kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila
gharama yoyote na kujikusanyia pointi. Mteja atakapomaliza kujibu
maswali ya bure atapata ujumbe utakaomuuliza kama angependa kujiunga na
ngazi ya premier, ili kuwezeshwa kufunguliwa maswali zaidi na
kujikusanyia pointi nyingi kwa zawadi zenye thamani kubwa.