Umeshawahi kujiuliza huwa inakuwaje pale wasanii ambao ni wapenzi na kimuziki wako kwenye kundi moja wanapokuwa na matatizo ya kimahusiano? Haikwepeki kwa couple yoyote kutofautiana kauli, kuudhiana , kugombana kiasi cha kutotaka kusemeshana, kitu ambacho kina changamoto kwa wasanii ambao ni wapenzi.
Mfano wa couple za namna hiyo kwa Tanzania tunao Jux na Vanessa, rapper One The Incredible na Grace Matata, Witnesz na Ochu Sheggy, Nuh Mziwanda na Shilole na bila kuwasahau Nahreel na Aika wanaounda kundi la Navy Kenzo.
Inawezekana isiwe shida sana kwa wasanii ambao ni wapenzi lakini lakini kila mmoja anafanya muziki wake kivyake na sio kundi, shida kubwa inakuja kwa wasanii wapenzi ambao wako kwenye kundi moja kama Navy Kenzo.
Waimbaji hao wa ‘Game’ inayofanya vizuri kwenye chati mbalimbali za Nigeria kwasasa, Navy Kenzo wanakiri kuwa hata wao huwa wanagombana kama wapenzi, lakini ugomvi wao haujawahi kuwaharibia kazi hata kama siku wamegombana wana show.
“Na sio kwamba hatujawahi kugombana, nadhani tumeshagombana tunaenda kwenye show, lakini mara nyingi huwezi kujua unakuta yaani tuna smile fresh tunakamua tunakumbatiana pale stejini yaani mzuka, halafu sisi hatujawahi kugombana zaidi ya masaa mawili yaani tunagombana halafu tunawekana sawa.” Nahreel aliiambia Clouds FM.
Aliongeza, “Unaweza kuta mtu ameshakulipa kwahiyo huwezi ukaharibu kwasababu ya mapenzi yenu,mnakamua tu kwanza show inatengeneza vitu vingi inatengeneza profile, mkiharibu show unakuta sasa mnajiharibia wenyewe show nyingne mnakuwa hampati.”
Kwa lugha ya kigeni hiyo inaitwa kuwa ‘professional’ kwa kutofautisha kazi na mahusiano binafsi ambayo hayawahusu mashabiki wa muziki wao.