Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali
yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye
wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi
nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe
mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo
amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
Sehemu
ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya
leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini
na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania
kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25
mwaka huu.
Mgombea
wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi
Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika
kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga
Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
Mmoja
wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za
CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa
kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora
waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema leo
jioni,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa
wananchi wa mji wa Tabora waliojazana kusikiliza Sera na Mipango ya
Chama Cha Mapinduzi itakayotumika kuongoza kwa miaka 10 ijayo.
Wananchi wakishangilia .
Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John
Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora.
Baadhi
ya Wakazi wa mji wa Simiyu wakisubiri kumsikiliza mgombea Urais wa
CCM,Dkt Magufuli kuwahutubia akitokea wilayani Nzega mapema leo mchana
Wafuasi
wa chama cha CCM sambamba na wananchi wa Uyui wakimsikiliza Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye
mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
Wafuasi
wa chama cha CCM wakiwa na Mabango yao ndani ya uwanja wa Ali Hassan
Mwinyi,wakimpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Sehemu
ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara
wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Tabora Ndugu Hassani Wakasubi akitoa ufafanuzi mfupi
kwenye mkutano wa kampeni wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye
uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora
Sehemu ya umati wa wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John
Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa
hadhara wa kampeni ndani ya uwanja wa Ali Hassa Mwinyi,mjini Tabora.
Wananchi wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia.