Wasanii
wenye vipaji vya kuimba wakihakiki majina yao kwa DJ Haazu, wa Radio 5
wakati wa mchakato wa RADIO 5 KAMATA KIPAJI uliofanyika katika viwanja
vya TP SINZA Jijini Dar es salaam Septemba 12, 2015.wenye lengo la
kusaka vijana wenye vipaji na kuwainua kutokana na vipaji vyao.
Katika
kuonyesha kuwa wapo karibu na vijana wa kitanzania katika kuwasaidia
kuwainua kiuchumi na kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini
mwa Tanzania ARUSHA Radio 5 kimenzisha mchato maalum wa kusaka vipaji
kwa vijana wa kitanzania mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam
ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanamuwezesha kijana mwenye kipaji
kufikia malengo na ndoto zake
DJ Haazu akiwajibika.
Radio
5 imekuwa na michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta
tofauti tofauti zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga
mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba
saport ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi,ujasiriamali na fani
nyingine.
Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao
umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA
KIPAJI katika viwanja vya TP sinza darajani ilishughudiwa vijana wengi
wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi
mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.
WAfanyakazi
wa RADIO 5 wakishangilia wakati Wasanii mbalimbali ambao ni vijana
wenye vipaji wakati wakionesha vipaji vyao jukwaaji (kulia), Mtangazaji
wa Redio 5 Mwangaza Jumanne (katikati), Meneja masoko na mawasiliano
Sarah Keiya na kushoto ni Meneja Vipindi, Mathew Philip.
Katika
zoezi hilo vijana walitakiwa kutuma nyimbo zao radioni ikiwa ni pamoja
na kujiandikisha majina yao ili siku waandaaji hao watakapofika katika
mtaa waliopo basi waweze kupata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao,na
kupatikana washindi ambapo mchakato huo utapita katika maeneo yote ya
jiji la Dar es salaam na mwisho kuwapata washindi wanne ambao ndio
watakaoibuka na zawadi kabambe.
Lengo kuu la mchakato huo ni kuwasaka vijana ambao wanavipaji na wapo
mtaani kutokana na sababu mbalimbali ambazo wameshindwa kuonyesha vipaji
hivyo ambapo RADIO 5 wameamua kupita katika mitaa hiyo kuhakikisha kuwa
vijana hao wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji walivyo navyo kwa
watanzania.
Umati wa mashabiki waliojitokeza kushuhudia wasanii wenye vipaji jukaani.
Wakati
zoezi hilo likiendelea mtandao huu ulipata nafasi ya kuzngumza na
mkurugenzi wa RADIO 5 Bw ROBERT FRANCIS ambaye amesema kuwa ni jambo
jema kuona kazi hilo imeanza kwa amani na furaha hivyo watanzania
waendelee kuwaunga mkono huku akiwataka vijana mbalimbali wenye vipaji
mkoani Dar es salaam kuendelea kujitokeza maeneo mbalimbali ambapo ziezi
hilo litakuwa linafanyika pamoja na kuendelea kusikiliza Radio hiyo.
Naye
meneja vipindi wa RADIO 5 Ndugu MATHEW PHILIP Akizungumza na mtaandao
huu wakati zoezi hilo likiendelea amesema kuwa kupitia vipindi vya Radio
hiyo hasa vipindi vya kutafuta vipaji nyumba kwa nyumba Dar es salaam
vijana wataweza kuinua vipato vyao huku akisisitiza kuwa watanzania
waendelee kusikiliza RADIO 5 kwani kuna mambo mengi na mazuri
yanaendelea kuwajia.
Msanii akilimiki jukwaa.
Meneja
biashara wa kituo hicho cha Radio Bi ANGELA MAINA alisema kuwa maana
halisi ya kufanya zoezi hilo ni kuwapa vijana nafasi ili kukuza vipaji
vyao hasa katika tasnia ya music ili miaka ijayo watanzania waone
matunda ya kazi hiyo haswa kwa washiriki wa zoezi hilo.
Aidha
meneja masoko na mahusiano wa RADIO 5 Bi SARAH LAZARO alisema kuwa
pamoja na lengo kuu la mchakato huo ni kuvumbua na kunyanyua vipaji
lakini pia ni nafasi kwa wadau wa biashara na mashirika binafsi haswa
yanayojihusisha na maswala ya kijamii kuanza sasa kushirikiana na radio 5
ili kukuza biashara zao na kushiriki katika kuendeleza jamii.
Mtangazaji wa kituo hicho Julius Kamafa.
Katika
mchakato huo endelevu utakao fanyika katika jiji la Dar es salaam
unataraji kuwapata washindi wanne wa mkoa huu ambapo washindi hao
watajinyakulia zawadi mbalimbali kama ifuatavyo
Mshindi
wa kwanza anataraji zawadi ya kurekord albam nzima bure kwenye studio
za kisasa na kupata promotion kubwa ya kazi yake,mshindi wa pili
anataraji kurekord nyimbo mbili bure pamoja na pamoja na promotion ya
miezi sita(6),mshindi wa tatu atapata kurekord nyimbo moja pamoja na
promotion ya miezi mitatu,huku mshindi wan ne ataweza kurecord nyimbo
moja pamoja na promotion ya mwezi mmoja.
Msanii Hance Mpozi kutoka Tegeta Dar es Salaam akionesha kipaji chake.
Mashabiki.
Wanii wa kundi moja wakimiki jukwaa.
Ni Msaga Sumu akitoa burudani.
Mtalamu wa kiduku.
Kulia ni DJ Haazu, pamoja na wasanii.
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja.
CHANZO:PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG