MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Sep 14, 2015

Makamua: Nina nyimbo zaidi ya 100 zipo ndani


Makamua1
Muimbaji wa R&B, Mack Paul Sekimanga aka Makamua amewataka mashabiki wa muziki wake kusubiria ujio wake mpya akiwa chini ya Mj Records.Makamua ameiambia Bongo5 kuwa, ana nyimbo zaidi ya 100 alizorekodi katika studio tofauti tofauti ila anachohitaji sasa hivi ni ujio mpya akiwa chini ya Mj Records.

“Nimefanya kazi na producers tofauti tofauti lakini mwisho wa siku nimekuja kuangukia MJ Records. Kwahiyo watu wasubiri kupata sound za ukweli kutoka MJ,” alisema Makamua.
“Hapa nilipo nina nyimbo zaidi ya 100 zipo ndani, kutoka katika studio tofauti tofauti, ila kwa sababu sasa hivi nimesaini mkataba na Marco Chali wa Mj Records, watu na mashabiki wa muziki wangu wasubirie vitu vikali zaidi.”

chanzo: Bongo5