Sep 14, 2015
Khajida Kopa atamani kuolewa tena
Malkia wa mipasho Tanzania na muimbaji ya TOT, Khadija Omari Kopa aliyefiwa na wake Jaffari Ally, Juni 2013, amesema huu ni wakati wa kutafuta mwanaume wa kumuoa. Akizungumza hivi karibuni na kwenye The Sporah Show, Khadija alisema atajisikia vizuri kama akimpata yule anayempenda.
“Nimeolewa kwa harusi zaidi ya mara na bado natafuta love, sitachoka. Raha ya maisha nikuwa na mtu anayekupenda,” alisema Khadija.
“Mimi nadhani mwanaume anayekuwa na mimi hatamani kuniacha, kwa jinsi ninavyoishi na mume wangu ni kama ndugu yangu, yaani naishi naye kwa mapenzi ya ukweli, sinaga mapenzi ya kubabaisha,” aliongeza.
“Na ninapenda kumchagua mtu ambaye nahisi kwenye moyo wangu ananigusa, nampenda ili nisimpe tabu, kwa sababu kama mtu unampenda hauwezi kumsumbua.
credit: Bongo5