Kampeni za uchaguzi zimewatengenisha maswahiba kwenye muziki, Nay wa Mitego na Diamond Platnumz.
Wawili hao waliohit na wimbo wao ‘Muziki Gani’ wapo kwenye kampeni za
pande mbili zenye nguvu kwenye uchaguzi wa mwaka huu, Ukawa na CCM.
Na sasa ubishani wao umehamia kwenye siasa.
Kupitia Instagram, Diamond amepost kipande cha video cha show yake ya
Zanzibar kwenye kampeni za chama cha mapinduzi na kuandika: Bado
wewe tu @naytrueboy kurudi nyumbani….kama
nayaona vile yale maselfie
yetu na nguo za kijaniblushlaughingsweat_smile #AboutYesterday.”
Nay amemjibu Diamond kwa kuandika:
Nimekataa siendi popote. Wanasema huu ndo muda wa Wasanii kupiga
hela ni kweli, ila mi kwangu itakua tofauti kidogo. Mi ni moja kati ya
Wasanii wachache wafanya biashara. Ila kwa kipindi iki cha uchaguzi
nimeweka pembeni kidogo maswala ya biashara now ni #Harakati huwezi
kumnunua mwanaharakati wa kweli coz ata pesa anajua kuitafuta nje ya
#Harakati. Uchaguzi ukiisha we leta izo Deal sasa za mamilioni mia
tutafanya, ila kwa sasa tunapigania Maslahi ya nchi na kile wanachotaka
watanzania Wengi. Naamini #Mabadiliko2015. @diamondplatnumz hujui
kusoma, ata picha huoni?! Watanzania wanataka #Mabadiliko2015.”