Sep 22, 2015
Mashavu kwa Tiffah hayajaja yenyewe tu, ni ubunifu wangu – Diamond
Makampuni makubwa hayajatangaza kupitia picha za kwanza za Diamond Platnumz, Latiffah hivi hivi. Kwa mujibu wa staa huyo ni ubunifu wake na proposal nzuri ndizo zimeyavutia.Diamond ameiambia 255 ya XXL kupitia Clouds FM kuwa yeye binafsi amepigana kuangalia mwanae atapata vipi deals zitakazomwingizia pesa.
“Wakati mwingine kama mzazi wasanii na celebrity lazima tuangalie tunajiongunisha vipi na makampuni. Tusiwe tunayalaumu tu makampuni haya support wasanii, lazima na wewe uwe creative,” amesema. “Uwe mzuri wa kuandika idea na kupeleka kwa watu tofauti tofauti.”
Aliongeza, “sisi tumepeleka na tukaifanyia presentation, wakasikiliza wakaona ina faida kwetu na kwao pia. Let’s say mtoto wako akiwa ni balozi wa bima ya kampuni yako itaongeza watoto kwa sababu kila mtu atajua kuna umuhimu gani wa mtoto kuwa na bima ya afya.”