Mmoja kati ya member wanaounda kundi la muziki la ‘Rockaz’, Mo Rocka
amesema mwenzao Quick Rocka ameshindwa kuitumia nafasi yake vizuri
kuwasaidia wasanii wa kundi hilo.
Akizungumza na Planet Bongo ya EATV jana, Mo alisema hapendezwi na tabia ya Quick Rocka kujifanya anajua zaidi.
“Baada ya kutoka na ile Bullet, [Quick] akawa anafanya vizuri na yupo
kwenye label nzuri alitakiwa aitumie vizuri mpaka kwetu sisi lakini
aliitumia vibaya. Mimi naomba nisiwazungumzie wengine, sikuona mfano
mzuri kutoka kwake kwamba hakufanya kama mimi au zaidi yangu mimi kwa
kusema nitawasaidia wenzangu na kuwaweka sehemu inayofaa.”
“Lakini alichokifanya ambacho mimi nilikiona na sikukipenda ni
kujiweka yeye kwenye hali ambayo yeye ndo anajua zaidi. Yeye ndio
anayeweza akasema hiki kiko sawa na kiwe hivyo hivyo,” alisema Mo
Rocka.
“Lakini kiukweli kabisa, kiundani kila mtu ana matatizo na wenzake na
ndio kitu ambacho kimechangia na kimevuruga sana, kwamba Rockaz ikawa
haionekani na mimi kama Mo Rocka nikawa pia sionekani. Wanisamehe mimi
ni binadamu nina majukumu na vitu vingi vimetokea hapa kati kati ambavyo
vikanichanganya lakini sasa hivi ni mtu ambaye naanza kuandaa mazingira
ya kumrudisha Mo Rocka.”