Sep 14, 2015
Miss America wamuomba radhi Vanessa Williams ni kwa kumlazimisha kuvua taji mwaka 1983
Vanessa Williams alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kushinda taji la Miss America
Wengi wenu bila shaka mlikuwa bado hamjazaliwa baada ya mwaka 1983 Vanessa Williams kujivua taji la Miss America. Na sasa waandaji wa shindano la Miss America wamemuomba radhi Vanessa Williams, ikiwa ni miaka 32 iliyopita baada ya kulazimishwa kuvua taji hilo.
Williams alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kushinda taji la Miss America lakini alijiuzulu baada ya jarida moja kuchapisha picha za utupu bila ruhusa yake.
“Nataka kuomba radhi kwa chochote kilichosemwa au kufanywa,” mwenyekiti mtendaji wa Miss America, Sam Haskell alisema.
Williams aliyekuwa akitokwa na machozi alisema maelezo hayo hakuyategemea na yalikuwa ya kuvutia.
Kwa sasa akiwa na umri wa miaka 52, amefanikiwa kuwa muigizaji mahiri. Mwaka 1992 alitoa pia wimbo uliohit duniani, Save the Best for Last na wimbo wake Colors of the Wind uliotumika kwenye soundtrack ya filamu ya Disney, Pocahontas ulimpa tuzo za Golden Globe, Grammy na Oscar.
Williams ni mrembo pekee aliyewahi kulazimishwa kujivua taji hilo.
Alialikwa tena kwenye shindano hilo baada ya kuombwa kuwa jaji.
“I have been a close friend to this beautiful and talented lady for 32 years,” Haskell aliuambia umati. “You have lived your life in grace and dignity, and never was it more evident than during the events of 1984 when you resigned. Though none of us currently in the organization were involved then, on behalf of today’s organization, I want to apologize to you and to your mother, Miss Helen Williams. I want to apologize for anything that was said or done that made you feel any less than the Miss America you are and the Miss America you always will be.”
Naye Vanessa alisema: Thank you so much, Sam, so unexpected but so beautiful. I did the best that I could as Miss America in 1983 to 84. On behalf of my family, my mother in particular; [publicist] Brian Edwards, who orchestrated this entire thing to bring me back; and your leadership, your integrity and you bringing this pageant back to what it ought to be. I love you. I love the girls. And I’m so honoured to be back.”