Sep 17, 2015
Picha: Flaviana Matata na Rosemary Kokuhilwa wajichanganya na Paris na Nicky Hilton kwenye New York Fashion Week
Kutoka Kushoto, mwanamitindo Tori Praver, Paris, Nicky na Flaviana Matata
Mrembo wa kimataifa kutoka Tanzania, Flaviana Matata pamoja na stylist wa Tanzania aishiye nchini Marekani, Kokuhilwa Rosemary Jumanne hii walijichanganya na mastaa wengine kwenye New York Fashion WeekFlaviana ambaye hivi karibuni alifunga ndoa naye pia anaishi jijini humo.
Wawili hao walijikuta wamekaa kwenye mstari wa mbele na madada matajiri wa Hilton Hotel, Paris Hilton, 34 na Nicky Hilton Rothschild wakati mbunifu wa mavazi, Dennis Basso alikua akionesha nguo zake za mwaka 2016.
Kwenye mstari huo alikuwepo mrembo, Tori Praver.
Chanzo: Daily Mail