Sep 17, 2015
Facebook kuanza majaribio ya button mpya ya ‘dislike’ hivi karibuni– asema Mark Zuckerberg
Mwanzilishi wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema kuwa wanalifanyia kazi ombi la kuongeza button ya ‘dislike’ ambayo imekuwa ikiombwa na watumiaji wengi wa mtandao huo.Mark amesema kuwa muda si mrefu wataanza kuifanyia majaribio button hiyo;
“Tumewasikia na tunaifanyia kazi na tutawaletea kitu kitakachokidhi mahitaji ya jamii kubwa. Watu wamekuwa wakiulizia kuhusu button ya ‘dislike’ kwa miaka mingi, na leo ni siku maalum napenda kusema tunaifanyia kazi na muda si mrefu tutaanza kuifanyia majaribio. alisema Zuckerberg.
Ameongeza kuwa kampuni yake inaamini kuwa watu hawataitumia alama hiyo kwa ubaya,
“Sio kila muda ni muda mzuri. Kama ukishare kitu cha kusikitisha kinachokugusa kama kufiwa na mwanafamilia, haitakuwa vizuri kulike post hiyo, nadhani ni muhimu wa kuwapa watu option nyingine zaidi ya kui-like hiyo post.”