Mkuu wa usalama wa mahali pa kazi wa TBL Mbeya, Godfrey Kisulilo akiwaonesha waandishi wa habari namna ya kutunza maji.
Waandishi wa habari Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza ziara katika kiwanda cha bia cha TBL Mbeya.
WAFANYABIASHARA
mkoani Mbeya wamehimizwa kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda cha bia cha
TBL mkoani kwao kwa kujihusisha na biashara zenye mahusiano na kiwanda
hicho ili waweze kunufaika na uwepo wake.
Miongoni mwa fursa zilizopo ni pamoja na kuanzisha viwanda kwaajili ya kusaga unga wa mahindi utumikao katika kutengenezea bia.
Meneja
wa kiwanda cha TBL Mbeya Waziri Jemedari alitoa hamasa hiyo
alipozungumza na wanahabari mkoani hapa kwenye shindano la kuonja na
kutambua ladha ya bia lililofanyika kiwandani na kuwashirikisha
wanahabari kutoka vyombo mbalimbali.
Jemedari
alisema bado wafannya biashara na wakulima mkoani Mbeya hawajaitumia
vyema fursa ya uwepo wa kiwanda hicho hatua inayopelekea wenzao kutoka
maeneo ya mbali kunufaika na fursa hiyo.
Alisema
licha ya mkoa wa Mbeya kuwa miongoni mwa mikoa inayozalisha kwa wingi
mahindi,bado kiwanda hicho kinalazimika kuagiza unga kutoka
Arusha,Iringa,Kibaigwa na Dar es salaam.
“Wafanyabiashara
wa Mbeya bado wamejikita katika biashara nyingine ikiwemo ya kununua
nafaka kutoka kwa wakulima na kuziuza tena pasipo kuziongezea
thamani.Hii inatulazimu kuagiza unga wa mahindi wa dona kutoka mbali
wakati hapa mahindi yanalimwa kwa wingi.”
“Nadhani
hawajatambua uwepo wa kiwanda hiki unavyoweza kuwanufaisha.Hatuwezi
kufungua viwanda vya kusaga unga wa dona kwakuwa tutakuwa tunawanytima
wengine fursa.Sisi tunatengeneza bia,tunahitaji wadau wengine wa
kutuzalishia malighafi za kulisha kiwanda chetu” alisisitiza.
Alisema
kwa sasa mahitaji ya unga wa mahindi wa dona kiwandani hapo ni mkubwa
ambapo jumla ya tani 30 hutumika kwa kila juma moja hivyo ni fursa nzuri
kwa watakaopenda kuwekeza kwenye uzalishaji wa malighafi hiyo.
Alisema
TBL iko tayari kukutana na mfanyabiashara yeyote atakayeonesha nia ya
kuwekeza katika biashara hiyo na itahakikisha inampa mwongozo juu ya
namna gani malighafi inayohitajika na kiwanda inavyopaswa kutengenezwa.
Aliitaja
fursa ya kilimo cha Shayiri kuwa faida nyingine ambayo wakazi wa Mbeya
hawajawekeza ipasavyo kwani hadi sasa kwa mkoani hapa ni wakulima wa
wilaya ya Mbozi pekee wanaozalisha huku kiwanda kikilazimika kununua
bidhaa hiyo kutoka maeneo mengine ikiwepo Sumbawanga mkoani Rukwa.
Alisema
licha yak ampuni kutoa fursa ya kuwawezesha wakulima katika shughuli
mbalimbali za uzalishaji wa zao hilo,bado mwitikio wa wakulima mkoani
hapa ni mdogo mno katika kilimo cha zao la Shayiri wakati soko ni la
uhakika.
Katika
shindano la kuonja bia,mtangazaji wa Mbeya FM David Nyembe aliibuka
mshindi akifuatiwa na mwakilishi wa ITV mkoani hapa Emmanuel Lengwa
aliyeshika nafasi ya pili.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA