Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Wakati shule zote za serikali na za binafsi nchini Kenya zikianza
kufungwa kuanzia hii leo, rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta akihutubia
taifa hilo kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa serikali yake haina
uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara wanayodai waalimu wanaoendelea na
mgomo.
Mgomo wa walimu nchini Kenya
Ametoa wito kuwa, mgogoro huo utatuliwe kwa amani na kusema kuwa
shule zote zinafungwa kuanzia leo. Serikali ya Kenya imeagiza shule zote
nchini humo zifungwe kuanzia leo huku mgomo wa walimu nchi nzima
ukiendelea.Barua kutoka kwa wizara ya elimu imeagiza shule zote za serikali na za kibinafsi zifungwe na wanafunzi warudi majumbani mwao. Watakaosalia shuleni pekee ni wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kitaifa ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu.