Mwenyekiti
wa Tamasha la 34 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni, John Mponda
(katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam leo, kuhusu tamasha hilo litakalofanyika kuanzia tarehe 21 hadi
27, 2015 katika Kumbi na Viunga vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBa), mkoani Pwani. Kulia ni Katibu wa Tamasha hilo na
Ofisa Biashara, Benjamini Malimbali na Ofisa Habari, Sophia Mtakajimbo.
Hapa Mwenyekiti
wa Tamasha hilo, John Mponda (kulia) akisisitiza jambo kuhusu tamasha
hilo. Kushoto ni Ofisa Habari wa Tamasha la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa).
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
TAMASHA la
kimataifa la sanaa na utamaduni Bagamoyo liliasisiwa mwaka 1981 na Chuo cha
Sanaa Bagamoyo ambacho kwa sasa ni Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo.
Lengo kuu la Tamasha kwa wakati huo ilikuwa ni kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo
cha sanaa kuonyesha kwa vitendo yale waliojifunza kwa mwaka mzima kwa
kuwashirikisha wakazi wa Bagamoyo, baada ya Tamasha hilo kufanikiwa uongozi wa
chuo uliamua tamasha hilo lifanyike kila mwaka kwa kushirikisha Vikundi mbalimbali
vya ndani na nje ya nchi ili kubadilishana Uzoefu na hivyo kujizolea umaarufu ndani na nje ya
Tanzania.