UMEME WA PUMBA ZA MCHELE, MASHUDU YA PAMBA WATUMIKA KUENDESHEA MITAMBO YA TBL MWANZA
Meneja
wa kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Mwanza, Raymond
Richmond,akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampuni hiyo kutumia
mapumba ya mchele na mashudu ya pamba,kama chanzo cha nishati ya umeme
kinachotumika kuendeshea mitambo.Kushoto ni Meneja wa Maji na Nishati wa
kampuni hiyo, Sunday Kidolezi.
Meneja
wa kiwanda cha Kampuni ya Bia (TBL) Mwanza, Raymond Richmond,
akizungumzia mradi wa matumizi ya mapumba ya mchele na mashudu ya
pamba,ambacho ni chanzo cha nishati ya kuendesha mitambo kiwandani
hapo.Nishati ni rafiki wa mazingira kwa sababu haina hewa ukaa.Wanaokoa
Dola za Kimarekani (USD) 400,000 hadi 500,000 kwa mwaka ambazo
zingetumika kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendeshea mitambo .
Waandishi
wa habari wakiongozwa na Meneja wa Kiwanda cha kampuni ya Bia (TBL)
Mwanza, Raymond Richmond(wa kwanza kushoto), kwenda kutembelea mtambo
unaotumia mapumba ya mchele na mashudu ya pamba kuzalisha nishati ya
umeme inyotumika kuendesha mitambo ya kiwanda hicho.Kulia ni Meneja wa
Maji na Nishati wa TBL, Sunday Kidolezi.