Mwenyekiti
wa National Governance Internet Forum ambaye pia ni Rais wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Kenneth Simbaya akiwakaribisha
wadau wa mitandao na watumiaji wa intaneti kwenye jukwaa hilo kabla ya
kumkaribisha mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA kufungua rasmi jukwaa
hilo.. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tanzania Education and Research
Network (TERNET), Amos Nungu na Kushoto ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano,
Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph akifuatiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi
Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday Richard. (Picha
zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi Mwetu
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, (UNESCO),
limewaomba wadau wa habari hasa wa matumizi ya intaneti kuzingatia
maadili na usiri katika kazi zao ili kutovunja sheria zilizowekwa na
mamlaka husika likiwemo suala la sheria ya mtandao iliyopitishwa hivi
karibuni nchini Tanzania.
Hayo
yameelezwa na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika
la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin
Yusuph aliyekuwa akimwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO, Zulmira Rodrigues
katika Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya mtandao (NIGF),
lililofanyika mwishoni mwa wiki na kuandaliwa na Umoja wa Klabu za
Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).
UNESCO
inaamini masuala ya usiri katika mitandao ni njia bora zaidi za
kuepukana na suala la mmomonyoko wa maadili na usio zingatia taaluma.
Ambapo
amebainisha kuwa, takribani Asilimia 84 ya Mataifa duniani wamegundua
hawana sheria madhubuti ya kulinda uhuru wa usiri kwa wananchi kupitia
mitandao hivyo ni muhimu kuzingatia taaluma na maadili kwenye matumizi
ya intaneti hasa kwa kipindi hichi.
“UNESCO
inaamini mambo muhimu ya kuzingatia juu ya matumizi ya mitandao ikiwemo
kuwa na Uwazi, Upatikanaji na Ushirikishi. Kwa hayo machache, mjadala
huu wa matumizi ya mtandao unaweza kufanikiwa na sie tunapenda kuungana
na nyinyi katika kushirikiana katika suala hili” alieleza Ofisa Miradi
ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi,
Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. Sunday
Richard akifungua rasmi Jukwaa la wadau wa usimamizi wa masuala ya
mtandao (NIGF) lililoandaliwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari
Tanzania (UTPC) na kufanyika mwishoni mwa juma katika ukumbi wa mikutano
COSTECH jijini Dar.
Kushoto
ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph
aliyemwakilisha Mkurugenzi wa UNESCO na kulia Mwenyekiti wa National
Governance Internet Forum, Kenneth Simbaya.
Aidha,
katika mkutano huo, imeelezwa kuwa, matumizi makubwa ya mtandao wa
kompyuta (intaneti) yatasaidia ongezeko la pato la taifa (GDP).
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya jukwaa la
mtandao wa intaneti (IGF) Kenneth Simbaya wakati wa jukwaa hilo ambapo
amebainisha kuwa, katika matumizi yake ni muhimu sana kujadili
kutengeneza kesho wanayoitaka watanzania katika matumizi ya mtandao.