Bw.
Moustafa H. Khataw kutoka kampuni ya Skylink akiwakaribisha waandishi
wa habari pamoja na wageni waliofika katika droo ya kuwapata washindi
wanne leo kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa
ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Bw.Husain
AlSafi kutoka Emirates ambao walikuwa ni wadhamini wa shindano akiongea
na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo katika ofisi za Skylink.
Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Bw. Abdallah Hemed akizichanganya vipeperushi ili kuwapata washindi wa droo hiyo.
Mwandishi
wa habari kutoka TBC akiwa ameshika moja ya kipeperushi cha mteja wa
Skylink aliyeibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia gari mpya aina
Hyundai ix35 katika droo iliyochezeshwa kwenye ofisi za Skylink
Jijini Dar es Salaam.
Ofisa wa Skylink Solomon Mwale akiwatangaza washindi waliopatikana kwenye droo iliyofanywa na kampuni ya Skylink leo.