Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na tuzo yake kutoka MTV EMA.
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ jana ametwaa
tuzo ya MTV EMA katika kipengele cha ‘Best Worldwide Act: Africa/India’
akimgalagaza Miss World 2000, Priyanka Chopra. Diamond alikuwa akichuana
na muigizaji wa filamu na aliyekuwa Mrembo wa Dunia (Miss World 2000),
Priyanka Chopra katika tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA) kwenye
kipengele hicho.
Miss World 2000, Priyanka Chopra.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Diamond amewashukuru sana
mashabiki wake, wasanii wenzake, uongozi wake pamoja na familia yake
huku akisema kutokana na zoezi la uchaguzi mkuu hapatakuwepo na mapokezi
makubwa ila itaandaliwa siku maalum kwa ajili ya kupiga picha na tuzo
hiyo. Hivi ndivyo Diamond alivyoandika: Tuzo hizo zilitolewa jana Oktoba 25, 2015 jijini Milan, Italia.