Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles
Mkumbo akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana ambapo alitoa
msimamo wa jeshi hilo juu ya suala la wananchi kubaki mita 200 kutoka
vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura siku ya jumapili
Octoba 25,2015 ikiwa ni siku ambayo Watanzania watashiriki katika zoezi
la Uchaguzi Mkuu wa Kuwachagua Wawakilishi wao kuanzia ngazi ya
Madiwani, Wabunge na Rais.
Kamanda
Mkumbo alisema kuwa jeshi la polisi linawataka wananchi wote kurejea
majumbani mwao baada ya kupiga kura badala ya kubaki mita 200 kutoka
vilipo vituo vya kupigia kura kama ambavyo baadhi ya viongozi wa vyama
vya kisiasa wamekuwa wakiwashauri kwa ajili ya kulinda kura.
Alisema
Jeshi hilo linapiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote siku hiyo ya
uchaguzi na kwamba litawachukulia hatua kali wale wote watakaoonekana
kwenda kinyume na agizo hilo ikiwa ni pamoja na kuvaa sare za vyama vya
siasa ama kuonyesha ishara zozote za vya hivyo.
Wakati
huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP.Ernest Mangu nae ametoa
tamko kama hilo akiwataka watanzania kurejea majumbani baada ya zoezi la
kupiga kura akisema kuwa jeshi hilo limejipanga kuhakikisha kuwa
linaimarisha usalama kwa wananchi watakaokuwa wakitoka majumbani kwenda
kupiga kura na kurejea majumbani mwao.
Hata
hivyo Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es salaam hii leo
inatarajia kutoa maamuzi yake juu ya suala hilo la uhalali wa wananchi
kubaki umbali wa mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya
kupiga kura.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo
Mwanahabari
Wanahabari
chanzo na Na:George Binagi-GB Pazzo, BMG