Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akimkaribisha
ofisini kwake Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania
kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando
Emilio Guebuza. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (Katikati kulia)
akimfafanulia jambo Mkuu wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania
kutoka Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zamani wa Msumbiji, Mhe Armando
Emilio Guebuza (wapili kushoto), pamoja na wajumbe wenzake, jinsi
Tanzania ilivyojipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25 mwaka huu utakavyokuwa wa amani. Wakwanza kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu
wa Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania kutoka Umoja wa Afrika
(AU), ambaye pia ni Rais wa Zamani wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza
(kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (kushoto) wakati Mkuu huyo pamoja na wajumbe wenzake
walipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake kwa lengo la kujadili
masuala mbalimbali ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25
mwaka huu, hata hivyo, Chikawe aliwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utakuwa
wa amani. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
chanzo: JIACHIE