Oct 29, 2015
Muongozaji wa filamu wa Tanzania atajwa kuwania tuzo za Marekani
Muongozaji wa filamu wa Tanzania, Timoth Conrad ametajwa kuwania tuzo za Marekani, California Online Viewers Choice Awards.Pia filamu yake Dogo Masai imechaguliwa kuwania tuzo hizo zitakazofanyika jijini Los Angeles. “Nimechaguliwa kuwania tuzo ya BEST DIRECTOR na pia filamu ya Dogo Masai inawania BEST FEATURE FILM,” ameandika kwenye Facebook.
“Ninaomba sapoti yenu katika kunipigia. Unaweza kunipigia kura kadri uwezavyo hakuna limit.”
Kumpigia kura bofya hapa.
Hivi karibuni, Conrad alishinda tuzo zingine nchini Marekani.