MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Oct 29, 2015

SABABU 8 ZAFUTA UCHAGUZI ZANZIBAR!


Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha .
MBAYA! Huku Watanzania wakiwa na shauku ya kujua mbivu na mbichi juu ya matokeo ya uchaguzi mkuu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) imetangaza rasmi kuufuta uchaguzi huo na matokeo yake hadi pale itakapotangazwa upya huku sababu nane zikitajwa kusababisha.
Akizungumza na waandishi wa habari jioni jana visiwani Zanzibar, mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salum Jecha alizitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na kutofahamiana kwa baadhi ya wajumbe ndani ya chumba cha kutolea matokeo hali iliyowasukuma miongoni mwao kuvua mashati na kuanza kurushiana ngumi.

Pia, Jecha alisema sababu nyingine ni baadhi ya wajumbe kubainika kuwa ni wawakilishi wa vyama hivyo kushindwa kufikia muafaka stahiki juu ya zoezi hilo.Sababu nyingine ni kuwepo kwa kasoro za baadhi ya vituo, hususan Kisiwa cha Pemba, kuzidishwa kwa idadi ya kura kuliko idadi kamili ya jumla ya wananchi waliojitokeza kupiga kura.
Aidha, akionesha uso wa masikitiko, Jecha alitaja sababu nyingine kuwa ni kuhamishwa kwa masanduku ya kura na kuhesabia kura nje ya vituo husika. Mbali na hapo, sababu nyingine ni kutolewa nje kwa baadhi ya mawakala wakati wa utekelezaji wa zoezi la kuhesabu kura, hususan wale wa Chama cha Tadea.
Sababu nyingine ni pamoja na kuvamiwa baadhi ya vituo vya kuhesabia kura katika maeneo mengi, kitendo cha baadhi ya vyama vya siasa kuingilia kazi ya tume hiyo ikiwemo kutangaza matokeo, jambo ambalo Jecha alisema ni kinyume cha utaratibu na sheria ya uchaguzi.
Sababu nyingine ni malalamiko yaliyokithiri kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa huku sababu ya mwisho ni kufutwa kwa namba kwenye baadhi ya fomu na kuwekwa nyingine.“Kwa mantiki hiyo, kutokana na mamlaka niliyopewa kisheria, nikiwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, natangaza rasmi kufuta uchaguzi wote uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, pamoja na matokeo yake yote kwa upande wa Zanzibar, hadi pale tutakapotangaza upya,” alisema Jecha.
Hata hivyo, Chama cha Wananchi (Cuf) kimetoa tamko kukisema hakitambui kufutwa kwa matokeo hayo kwa vile Jecha ameamua mwenyewe bila kufuata taratibu za kisheria ambapo wao Cuf hawajapewa taarifa rasmi.