Akitangaza uamuzi huo mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Bw. Lubuva ametolea mfano wa kusimamishwa kwa uchaguzi Tz Bara wa mwaka 2005 baada ya mgombea mwenza NCCR Mageuzi Ali Omar Juma kufariki dunia ambapo uchaguzi Zanzibar uliendelea kama kawaida.
Ifuatayo ni sehemu ya barua toka Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)...
Akiongea
baada ya kutolewa tangazo hilo, Katibu Mkuu wa CUF na ambaye alikuwa
mgombea wa kiti cha urais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema
hatambui uamuzi huo kwani mwenyekiti wa tume hana mamlaka ya kuamua bila
kuwashirikisha makamishina.
Maalif Seif amesema wanawasiliana na taasisi za kimataifa na msaada juu ya jambo hilo.
Pia baada ya
kutolewa kwa uamuzi huo na ZEC, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
wamekutana na waandishi wa habari na kusema kuwa hawatakubali matokeo
yanayoendelea kutolewa na NEC.
Hata hivyo,
CCM kupitia Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za chama hicho, January Makamba
amesema ni vema wanasiasa wakawana utaratibu wa kupokea na kukubali
matokeo na kwamba anashangazwa na Ukawa kuanza kuonesha dalili za
kuyakataa matokeo.
Akitolea
ufafanuzi kuhusu uamuzi huo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema hilo halitaadhiri uchaguzi wa
rais wa Jamhuri ya Muungano.