Mgombea wa ubunge wa Ilemela kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Angelina Mabula.
Na Mwandishi WetuWAMEAMUA! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia wananchi wa mkoa wa Mwanza kuamua kumuengua mbunge Highness Kiwia huku Ezekiel Wenje wa Chadema (pichani) hadi tunakwenda mitamboni jana, alikuwa katika wakati mgumu wa kushindwa.
Staslaus Mabula.
Highness alikuwa akitetea Jimbo la Ilemela huku Wenje akitetea Jimbo
la Nyamagana ambapo kwa upande wa Ilemela, Angelina Mabula Chama Cha
Mapinduzi (CCM), aliibuka kidedea na Staslaus Mabula (CCM) akitajwa
kumpa wakati mgumu Wenje katika Jimbo la Nyamagana.Hata hivyo, katika jimbo la Ilemela, mbunge aliyepoteza nafasi yake, Kiwia aligoma kusaini hati ya matokeo, hali iliyopelekea vijana waliosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema kufanya fujo mitaani wakidai wakipinga matokeo na kusababisha jeshi la polisi kuingilia kati kuwatanya.
Pamoja na kuwa na asilimia kubwa ya kufanikiwa kurudisha viti vya Ilemela na Nyamagana vilivyokuwa mikononi mwa upinzani, maeneo mengine katika mkoa wa Mwanza, ndani ya majimbo ya Sengerema na Buchosa, ambayo yameendelea kubaki mikononi mwa CCM.
Aidha, katika hatua nyingine, katika Jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga, mgombea wa CCM, Jumanne Kishimba alimgaragaza vibaya James Lembeli aliyekuwa akiwania jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema, akitetea kiti chake, kabla ya kuhama CCM,
Mbali na majimbo hayo ya mkoa wa Mwanza, CCM imeendelea kuibuka na ushindi katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Geita, ambapo kwa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu alichaguliwa kuliongoza huku Joseph Kasheku Musukuma akilinyakua Jimbo la Geita Vijijini.
Pia, Lorensia Masere Bukwimba, ameendelea kulitetea Jimbo la Busanda ambalo ameliongoza kwa zaidi ya miaka mitano huku Hussein Kasu akilitwaa tena Jimbo la