Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefanya ziara ya
kushtukiza katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga ili kujionea
hali halisi jinsi huduma zinavyotolewa kwa wananchi siku moja tu baada
ya muuguzi wa kituo hicho kukamatwa kwa tuhuma ya kuiba dawa za
serikali.Pichani ni mkuu wa wilaya Josephine Matiro na katibu tawala wa
wilaya ya Shinyanga wakiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa wakiwa
wamepigwa butwaa baada ya kuona chumba kimesheheni dawa wakati mara kwa
mara wananchi wamekuwa wakiambiwa hakuna dawa badala yake wanaambiwa
wakanunue kwenye maduka ya watu binafsi mtaani-Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog .
Hapa ni ndani ya ofisi ya mganga mkuu/msimamizi wa kituo hicho ambapo
mkuu wa wilaya akiwa ameambatana na maafisa wengine wa manispaa ya
Shinyanga amekutana na uongozi wa kituo hicho pamoja na wananchi
waliomkamata muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila akituhumiwa
kuiba dawa za serikali.Kulia ni Rashid Shaban akimweleza mkuu huyo wa
wilaya jinsi walivyofanikisha kufichua wizi huo
Wa pili kutoka kulia ni msimamizi wa kituo cha afya Kambarage Dkt
Nassoro Yahya akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga kuhusu
suala la upungufu wa dawa katika kituo chake ambapo alisema kituo kina
upungufu wa dawa na walishatoa taarifa panapohusika siku nyingi
zilizopita.Hata hivyo maelezo yake yalipingana na yale ya kaimu mganga
mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana Raphael(mwenye suti pichani)
aliyedai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna tatizo la upungufu wa dawa bali
dawa pekee ambayo haipo ni ile ya Antibiotic
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kituo
cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine
amemwagiza mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kumsimamisha kazi muuguzi
Joseph Nkila anayetuhumiwa kuiba dawa za serikali pamoja na msimamizi
wa kituo hicho Dkt Nassoro Yahya kwa uzembe unaosababisha mwanya wa
upotevu wa dawa katika kituo hicho na kusababisha wananchi kuilalamikia
serikali kwa kukosa dawa wakati mkoa wa Shinyanga hauna tatizo la dawa