MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Nov 23, 2015

EAGT DODOMA WALITAKA TAMASHA LA SHUKRANI


  Mwenyekiti  wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la kumshukuru mungu kwa amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar na kuwahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za kiroho kutoka ndani ya nje ya nchi. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Khamis Pembe.

 KANISA la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) mkoani Dodoma limewataka waandaaji wa Tamasha la Kushukuru, Kampuni ya Msama Promotions kuukumbuka mkoa wa Dodoma katika tamasha hilo linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  mwishoni wa wiki jijini Dar, Mwenyekiti  wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama alisema amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mchungaji wa kanisa hilo mkoani Dodoma, Elia Meshack.

Msama alisema Mchungaji Meshack ameliomba tamasha hilo ili kufikisha asante yao kwa Mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Tanzania uliofanyika Oktoba 25 nchini kote.

Aidha Msama kwa kuwa waliandaa tamasha la kuombea amani uchaguzi Mkuu, hapana budi kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kuomba amani katika uchaguzi huo.

“Nimezungumza na Mchungaji Meshack akinieleza kwamba itakuwa vema Tamasha la Shukrani nikilifikisha mkoani Dodoma, Kamati yangu inafanya mikakati ya kuweza kufikisha asante kwa Mungu,” alisema Msama.