Waziri Mkuu mpya Mh. Kassim Majaliwa.
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha
jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu
wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa
Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli.
Mh. Majaliwa amepitishwa kwa kura 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote za ndio.