Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akionyesha simu aina ya Magnus
Bravo Z10 iliyo na ofa ya kifurushi cha kuanzia cha bure chenye dakika
150 za kupiga simu, SMS 150 pamoja na kifurushi cha internet chenye
ujazo w MB 150 kila mwezi kwa muda wa mienzi 6 katika uzinduzi wa
Smartphone Bazaar iliyopo Mlimani City. Pichani ni wafanyakazi wa
kitengo cha huduma kwa wateja wa Airtel
Moja
ya wateja waliotembelea Smartphone Baazar Mlimani City akijipatia simu
yake aina ya Magnus Bravo Z10 iliyo na ofa ya kifurushi cha kuanzia cha
bure chenye dakika 150 za kupiga simu, SMS 150 pamoja na kifurushi cha
internet chenye ujazo w MB 150 kila mwezi kwa muda wa mienzi 6 toka kwa
watoa huduma wa Airtel Bi Zainab Hamidu. Airtel imezindua Smartphone
Bazaar katika msimu huu wa sikukuu ili kuwawezesha watanzania kupata
simu bomba za kisasa kwa bei nafuu.
Meneja
kitengo cha huduma za Internet na simu , James Kagashe (wa kwanza
kushoto) akiongea na wateja mbalimbali waliotembelea Airtel Smartphone
Bazaar katika eneo la mlimani city kujipatia simu bomba na za kisasa
zenye ofa za vifurushi vya muda wa maongezi, sms na intaneti kwa gharama
nafuu.
- Yazindua smartifonika ofa yenye vifurushi vya bure kwa muda wa mienzi 6
- Wateja kupata ofa za simu za kisasa maeneo ya mlimani city na quality center kuanzia ijumaa hadi Jumapili
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa
mara nyingine imekuja na ofa kabambe kupitia SMARTFONIKA Bazaar na
kuwawezesha wateja kupata simu mbalimbali za kisasa katika msimu huu wa
sikukuu
Gulio la simu yaani smartphone Bazaar
litakuwa katika maeneo ya Mlimani City na Quality Center kuanzia siku ya
Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Watanzania watapata nafasi ya kuchagua na
kununua simu za aina ya smartphone inayokidhi mahitaji yao kwa bei
nafuu. Ofa hii pia itapatikana katika maduka ya Airtel nchi nzima.
Akiongea kwa niaba ya Airtel, Meneja
Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando alisema” Tunayo furaha kutambulisha
ofa hii kabambe katika msimu huu wa siku kuu itakayowawezesha wateja
wetu kununua simu kwa matumizi yao binafsi na kwaajili ya wapendwa wao
kwa bei nafuu kuliko zote sokoni.
Simu zitakazopatikana katika Smartphone
Bazaar ni pamoja na simu aina ya Magnus Bravo Z10 inayokuja na
kifurushi cha kuanzia cha bure chenye dakika 150 za kupiga simu, SMS 150
pamoja na kifurushi cha internet chenye ujazo w MB 150 kila mwezi kwa
muda wa mienzi 6 kwa gharama ya shilingi 75,000/=. Magnus Z10 ni simu
yenye screen kubwa inayomuwezesha mteja kuona taarifa mbalimbali kwa
urahisi zaidi battery yake inadumu kwa muda mrefu
Sambamba na simu ya Magnusa Bravo Z10
wateja wetu watapata simu mbalimbali za kisasa za aina ya Samsung,
Huawei, Tecno na Star times ambapo wateja wakinunua watapata ofa kabambe
kutoka Airtel.
“Tunaamini simu hizi zitakuwa simu
muafaka kwa watumiaji wa mara ya kwanza wa simu aina ya smartphone
kuweza kupata uzoefu tofauti na kufurahia huduma mbalimbali ikiwemo
huduma ya internet toka Airtel.
Natoa wito kwa wateja wetu kuwa wakwanza
kupata simu hizi za kisasa kwa kutembelea maduka yetu na gulio la simu
katika maeneo ya mlimani city na Quality center kila mwisho wa wiki.”
Aliongeza Mmbando