MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Nov 23, 2015

Zidane kajibu kuhusu kurithi nafasi ya Benitez Real Madrid, Rais wa klabu hiyo huenda akafanya maamuzi magumu Nov 23…

Bado headlines za Real Madrid kufungwa goli 4-0 katika uwanja wake wa nyumbani waSantiago Bernabeu dhidi ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona zinzazidi kuchukua nafasi, mchezo huo wa El Clasico ambao umeonekana kuwatawanya mashabiki wa Real Madrid pande mbili tofauti, wengine wakiamini kufungwa ni hali ya mchezo ila wengi wao wanaamini ni mbinu mbovu za Rafael Benitez.
Kabla ya mchezo wa El Clasico kuchezwa kulikuwa na stori kuwa Real Madrid kama watafungwa na FC Barcelona walikuwa wanatajwa kuwa huenda wakamfukuza Benitezna nafasi yake ya itachukuliwa na kocha wa kikosi cha wachezaji wa akiba wa Real Madrid (Castilla) Zinedine Zidane kitu ambacho Zidane amekanusha hadi sasa kurithi nafasi hiyo na kuwa yeye ni kocha na anafurahia nafasi yake ya kukifundisha kikosi cha akiba.
article-2613819-1D4DD7F000000578-399_634x423
Zinedine Zidane
“Mimi ni kocha wa Castilla lakini Benitez ni kocha wa kikosi cha kwanza cha Real Madrid na mambo yako sawa na ninafuraha kuona tunafanya vizuri na kikosi changu cha Castilla dhidi ya wapinzani wetu ambao tumekuwa tukicheza dhidi yao, kiukweli kama kocha nina mengi ya kujifunza siku hadi siku na bado sijakamilisha vyote” >>> Zidane

Hata hivyo kauli ya Zidane bado haijitoshelezi kuhusu yeye kutorithi nafasi ya Rafael Benitez ila wengi wanasubiri majibu ya Rais wa Real Madrid Florentino Perez ambaye jioni ya November 23 ameitisha kikao cha bodi na baada ya hapo ataitisha press conference na waandishi wa habari, hivyo tunaweza kusikia chochote kikitokea kwani hali sio nzuri katika jiji la Madrid, mashabiki bado wamechukizwa na mbinu za Benitez za timu kujihami zaidi kuliko kucheza mpira.
MD88. Madrid, 20/09/05.- El presidente del Real Madrid, Florentino Pérez, durante la rueda de prensa que ha ofrecido esta tarde en las instalaciones del estadio Santiago Bernabéu, en la que ha confirmado que el Real Madrid ha decidido no impugnar el partido que el pasado domingo perdió ante el Espanyol en Montjuic (1-0). EFE/Angel Díaz
Rais wa Real Madrid Florentino Perez ambaye ameitisha mkutano wa bodi jioni ya November 23 na baada ya hapo atafanya mkutano na waandishi wa habari
chanzo: Milad Ayo