Meneja
Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi
(kushoto) akizungumza na wanahabari wakati wa kutangaza mpango wake wa
‘GAPCO Safari Loyalty ‘, unaolenga kuwanufaisha wateja wake kwa kuwapa
mafuta ya bure, ulizindulia kwenye makao makuu ya Kampuni hiyo, Kurasini
jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa
Kampuni ya Mafuta ya GAPCO, Jane Mwita.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi
(kushoto) na Meneja wa Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Mafuta ya
GAPCO, Jane Mwita, wakionyesha vipeperushi vya Promosheni hiyo, mara
baada ya kuizindua rasmi.
Katika
kuelekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka huu, GAPCO, kampuni
inayoongoza kwa uuzaji wa mafuta, imeamua kuwapa wateja wake zawadi ya
kufungia mwaka. Katika kufanikisha hilo, kupitia mpango wake wa ‘GAPCO
Safari Loyalty programme ‘, kampuni imelenga kunufaisha na kuimarisha
uhusiano wa kudumu na wateja wake kwa kuwapa mafuta ya bure.
Mpango
huu unaoenda sambamba na promosheni ya ‘Jaza Mafuta na Ushinde’,
umedhamiria kutoa lita 4,000 za petroli au dizeli za bure kwa wateja 100
watakao bahatika ndani ya wiki nne. Katika droo za kila wiki, kutakuwa
na wateja 25 wanaoweza kujishindia lita 40 kila mmoja. Wateja wanaweza
kujiongezea nafasi za ushindi kwa kujaza mafuta mara nyingi zaidi.
Pia,
wateja ambao hawajajiunga na mpango wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme’
wanaweza kujiunga katika kituo chochote cha GAPCO kilichopo Dar es
Salaam ili waweze kushiriki katika promosheni. Motisha zinazotolewa
kupitia mpango huu, ni nje ya zawadi atakazoshida mteja katika
promosheni, mteja wa GAPCO atajikusanyia pointi zitakazomwezesha
kukomboa mafuta ya bure.
“Kupitia
mpango huu wa ‘GAPCO Safari Loyalty programme‘, tunataka wateja wetu
wawe na furaha na waendelee kutumia bidhaa na huduma zetu. Mbali na
kwamba tunatoa kadi hizi kwa mteja mmoja mmoja, pia tunaanzisha kadi
kwa ajili ya makampuni na wasafirishaji. Kupitia kadi hizi, mbali na
wateja kuweza kujikusanyia pointi zitakazomwezesha kupata mafuta ya
bure, wateja wetu wataweza kudhibiti matumizi ya fedha zao,” alisema
Meneja Masoko wa GAPCO, Caroline Kakwezi.
Mwanzoni
mwa mwaka huu, GAPCO ilifanya mabadiliko makubwa na kuamua kujikita
katika kujipambanua kwa namna ya kipekee. Katika mabadiliko haya, GAPCO
iliboresha muonekano na mazingira katika vituo vyake vya mafuta
vilivyopo Dar es Salaam. Ahadi ya kuwa na mafuta yenye ubora na ujazo
wakuaminika, mazingira mazuri na rafiki, huduma bora inayojali mteja na
ya haraka ni kati ya faida mahsusi anazopata mteja anayefika katika
vituo vya mafuta vya GAPCO nchini.
“Tukiwa
na mtazamo na nia ya kuwapa wateja wetu maili nyingi zaidi na tabasamu
zaidi, malengo yetu ya muda mrefu ni kuweza kupanua huduma zetu na
kuhakikisha tunatoa huduma za ziada ili kuwaachia wateja wetu kumbukumbu
sahihi ya huduma bora na za kisasa,” aliongeza Kakwezi.