Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akikabidhiwa zawadi ya shati la asili la Wamwera na Mzee Saidi Issa
Hanga katika mkutano wa hadhara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 20,
2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na
Mkewe Mary wakisalimiana na wazee wa Ruangwa kabla ya mkutano wa hadhara
uliohutubiwa na Waziri Mkuu mjini Ruangwa Desemba 20, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akionyesha na kufurahia silaha za asili alizokabidhiwa na wazee wa
Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini hapo Desemba 20,
2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
alipokea zawadi ya rungu kutoka kwa Mzee Issa Juma Nangalapa ikiwa ni
ishashara ya kumtaka awaadhibu wotw wanaokiuka sheria. Alikuwa katika
mkutano wa hadhara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 20, 2015.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifurahia moja kati ya zana na silaha za asili alizokabidhiwa na wazee
wa Ruangwa kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini hapo Desemba
20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)