Naibu
Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akizungumza
na wanahabari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam
leo kuhusuiana na mtandao huo kutanua huduama zake hadi kufikia asimimia
95 ya watazanzania. Wanaoshuhudia ni Naibu Mkurugenzi wa Rasilimali
Watu, Emanuel Malyeta (kushoto), na kulia kwake ni mwanasheria wa
kampuni hiyo,Christopher Masai.
Naibu
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Halotel, Emanuel Malyeta akifafanunua
jambo kwa waandishi wa habari. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Kampuni
ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai kulia kwake ni mwanasheria wa
kampuni hiyo,Christopher Masai.
Naibu
Mkurugenzi wa Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, Le Van Dai akimkabidhi
zawadi mwandishi wa gazeti la the Guardian, Sylivester Domaso.
Dar es Salaam, 5/1/2016: Kampuni
mpya ya simu za mikononi, Halotel, leo imetangaza mpango wake wa
kufikisha mtandao wa simu kwa asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu. Wakiongozwa na kauli mbiu yao ya Pamoja katika Ubora, wanalenga
kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na simu ya mkononi pamoja na kupata
huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa
imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo
havikuwa vimeunganishwa na huduma ya mtandao awali.
Hadi
sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka
sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano,
kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa
yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95%
ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.