MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 22, 2016

Kamati ya kuratibu Miss Tanzania yajitoa kwenye Mashindano

 Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo  jijini Dar-es-Salaam juu ya kujitoa kwao kama kamati ya kuratibu Miss Tanzania ambayo ilichagulia na kampuni ya Lino International Agency, kushoto ni Msemaji wa kamati hiyo Joketi Mwegelo na kulia ni Mjumbe wa kamati Gladys Shao .
Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Miss Tanzania Joketi Mwegelo akitoa maelezo  kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) namna Kamati hiyo ilivyokuwa ikijitahidi kubadili mfumo ili kubadilisha  muonekano wa mashindano ya urembo(Miss Tanzania) kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Pinto.
 Waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu mashindano ya Miss Tanzania, Juma Pinto (hayupo pichani) alipokuwa akitoa sababu za kujitoa kwa kamati katika mashindano hayo. PICHA NA Beatrice Lyimo-Maelezo.

Lilian Lundo- Maelezo,Dar es Salaam.

Kamati ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo tarehe 21/01/2016.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Juma Pinto alisema hayo leo, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.

“Tumekuja kutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni ya Lino International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya Miss Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya kamati kuingiliwa na kampuni ya Lino,” alisema Pinto.

Pinto aliongeza kwa kusema kuwa kamati yake ilipewa jukumu la kuendesha mashindano na kuwajibika kufanya kila kitu na Lino itakuwa kama washauri, lakini badala yake Lino imetaka kuhodhi majukumu yote na kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini.

Kamati hiyo imefanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na kubadilisha mfumo ili kuifanya Miss Tanzania kuwa na mwonekano tofauti kama ambavyo Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya ili kuboresha mashindano hayo.

Kutokana na kutopata muafaka katika vikao hivyo vya kuboresha mashindano ya Miss Tanzania, Kamati ya kuratibu mashindano hayo kwa nia njema na wala si kwa ubaya imeamua kujitoa katika Mashindano hayo.

Aidha, Pinto amewaomba radhi wadhamini ambao wameshaongea nao kama kamati na walioonesha nia ya kuwasaidia, amewataka kuendelea kufanya mawasiliano na kampuni ya Lino kwani madhumuni ni kudhamini mashindano na sio kamati.