MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 2, 2016

Kova astaafu akikumbuka matukio matatu

Kamanda wa kanda maalum ya jiji la  Dar es salaam Suleiman Kova leo ametangaza rasmi kustaafu  kulitumikia jeshi la Polisi nchini Tanzania.
Kova amesema hayo  leo alipokuwa akizungumza katika kipindi cha kumekucha cha ITV, ambapo  amesema  mkataba wake na jeshi la Polisi umeishia leo, hivyo analazimika kukaa pembeni katika kuitumikia jeshi hilo.
“Mmepata bahati sana, maana wakati nakuja Dar es salaam mwaka 2008 nikitokea Mbeya, kwa mara ya kwanza nilifanya kipindi hapa na leo hii nawaagia hapa, leo ndio siku ya mwisho kwangu kulitumikia jeshi la Polisi, mkataba wangu na jeshi la Polisi unaisha leo, lakini siwaachi hivi hivi, Kaimu wangu yupo atakuwa nanyi”, alisema Kamanda Kova.

Katika kipindi cha utumishi wake   Kova atakumbukwa kwa kufanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya kiuhalifu, wizi na uvamizi wa kwenye benki kwa kutumia silaha.