Mwana FA
Tayari msemo wa asanteni kwa kuja ambao
ni jina la ngoma mpya ya Mwana FA aliyoiachia hivi karibuni meeleweka
mitaani, unatumiwa na watu wengi kwa sasa, katika mitandao ya kijamii
ndiyo usiseme.
Ni swaga f’lani mtu akitaka kutupa dongo kwa ‘masnitch’ wake au kujibu mashambulizi akamalizia na msemo huo ‘asanteni kwa kuja.’
Ukweli ni kwamba kwa sasa msemo huo
ndiyo habari ya mjini, lakini mbali na kupaa kwake kitaani bado
mashabiki wengi wa muziki wamekuwa na maswali mengi juu ya maana halisi
ya wimbo huo.
Showbiz ilipiga stori na FA kufafanua baadhi ya vesi.
Ijumaa: Hongera kwa video kali ya
Asanteni Kwa Kuja uliyoiachia Jumatatu iliyopita, unaweza kuwaambia
wasomaji kuanzia audio mpaka video umefanyia wapi?
FA: Audio niligongea kwa Hermy B, B-Heat Records lakini kichupa nilifanya Sauzi kwa Spice Pictures.
Ijumaa: Asanteni Kwa Kuja imekuwa swaga
mpya kitaani, lakini kutokana na mashairi yake, wimbo unaonekana ni
dongo kwa msanii ambaye ni jamaa yako, funguka!
FA: Sijamlenga mtu yeyote hiyo ni idea tu, lakini kama yupo anayehisi unamhusu poa tu ni sawa na kurusha jiwe gizani.
Ijumaa: Sawa, hebu tucheki baadhi ya
mashairi, umeanza kwa kutaja neno ‘kwaya masta’ ulikuwa unamaanisha
nini? Au unamlenga nani?
FA: Hahaa! Hakuna, nilikuwa namaanisha mimi mwenyewe na uwezo wangu wa kuimbisha watu nikiwa
stejini.
Ijumaa: Kwenye verse ya kwanza kuna
mistari inasema;…sio salama sio salmini na silali ka vitani… hakuna
imani kwa masnitch mwana…njoo na panga ukute shoka ka’ zamani
zama…bastola na glasi ya vodka, lazima kuwa na adaka…madeni lazima
yalipwe hata mdaiwa
asipotaka’. Hapa inadaiwa umemtis GK, kuna ukweli?
FA: No, mimi na GK hatuna tofauti, yule
ni kama broo wangu, lakini niseme tu wazi asili ya Muziki wa Hip Hop ni
‘bato’ na sasa naona kama watu wamelala na hakuna ushindani.
Ijumaa: Vipi kuhusu mistari hii, dizaini
kama kuna mtu unamwambia; ‘wenye kelele wote sio Kings, kuwa na
nidhamu… tatizo la uongo ni kwamba milele haufiki mwisho…kaa kiporo
utatudanganya na kesho…malalamiko kibao ka’ mtoto wa kambo… kurukaruka
haijawahi kuwa dawa ya ulimbo…
FA: Ni kweli, mistari inajieleza,
niwasihi tu watu wasipende kuamini kila wanachokisikia na kuwachukulia
poa watu wanaoweza kuwarudisha nyuma kwenye harakati zao, ili kuwaonesha
kuwa unaweza fanya kweli.
Ijumaa: Tumalize na verse ya mwisho
kwenye hii mistari; ‘hata mi ni hater ka’ hunipendi hivyo hivyo
bro…ulete ubwege na nikupende mi ni Yesu?… hakuna shavu la pili toa
wembe nitoe kisu… bado mshabiki mkubwa wa kazi ya Mungu… ila kama
nakuweza simngoji nakupa kubwa wangu…life yangu movie na mi ndio
director… hata ukinielekeza sio kitu unakuwa extra…
FA: Hapo niliongelea udhaifu ninaoweza
kuwa nao kama mwanadamu, mtu akizingua pia nazingua, kikubwa najiamini,
maisha yangu nayaendesha mwenyewe, siwezi kufeli kisa mtu fulani
niliyekuwa naye hayupo