MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 14, 2016

WATUMISHI WAISHITAKI OFISI YA MKUU WA MKOA YA IRINGA KWA SSRA

 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya jamii, Sabato Kasuri akifafanua majukumu ya mamlaka hiyo kwa watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakati wakitoa dukuduku lao kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii
 Baadhi ya watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na idara zake wakifuatilia mjadala kuhusu mifuko ya hifadhi ya jamii ulioendeshwa na mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) mjini Iringa jana.

 WATUMISHI wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa na idara zake wameishtaki kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii wakiilalamikia kwa mambo makubwa matano ikiwemo ucheleweshaji wa mafao kwa wanachama wake wastaafu.

Katika kikao kilichofanyika juzi mjini hapa baina ya SSRA na watumishi hao; watumishi hao walisema uzoefu toka kwa baadhi ya wastaafu wengi unaonesha kwamba inawachukua muda mrefu kupata mafao yao.

Afisa Utumishi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa, Gasto Andongwisye alitoa mfano akisema; “baadhi ya watumishi waliostaafu kabla ya mwezi Julai mwaka jana hawajapata mafao yao hadi leo na imekuwa ni kilio kikubwa ofisini kwangu.”

Akijibu lalamiko hilo, Afisa Uhusiano wa SSRA, Sabato Kasuri alisema ucheleweshaji wa mafao ni changamoto ambayo tayari imefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa baada ya kubainika ilikuwa ikisababishwa na na ukosefu wa kumbukumbu sahihi za walengwa.