Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Asia (AFC) na Makamu wa Rais wa
FIFA, Sheikh Salman Bin Ebrahim Al Khalifa amewasili nchini leo mchana
na kupokelewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi.
Sheikh Salman amekuja nchini kwa matembezi ya siku ya mbili na atakua na mwenyeji wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Kesho
Jumanne, Sheikh Salman Bin Ebrahim Ali Khalifa atamtembelea ofisini
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa
Elisante Ole Gabriel.