ETIHAD
imetunukiwa tuzo ya kifahari ya “Uvumbuzi katika Usafiri” katika hafla
iliyoandaliwa na jarida la Travel Weekly ya kuwatunza wadau wa sekta ya
usafiri dunia nzima huko Uingereza maarufu kama “Globe Travel Awards”.
Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki kwenye hoteli maarufu ya
Grosvenor House, iliyopo Jijini London.
Kwa
kawaida tuzo hii hupewa kampuni ambayo imevumbua bidhaa au huduma yenye
kuleta wimbi la mabadiliko na maendeleo katika soko. Shirika la Etihad
waliibuka washindi baada ya jopo la wataalamu kuamua kwamba Shirika
linastahili tuzo hii kutokana na huduma yake ya “Makazi”- ambayo ni
huduma binafsi ya kipekee duniani yenye kutoa vyumba vitatu kwenye ndege
ya Etihad. Huduma hii, iliyoleta mapinduzi katika sekta ya usafiri wa
anga,ni matokeo ya programu ya utafiti na maendeleo iliyoendeshwa kwa
miaka saba na kusimamiwa na timu nzima ya ubunifu kutoka kituo cha
Uvumbuzi, Jijini Abu Dhabi.
“Makazi”
yanayopatikana kwenye ndege za Etihad aina ya Airbus A380 yana ukubwa
wa mita za mraba 11 na ndani yake kuna sebule, bafu la pembeni, chumba
kikubwa cha kulala na mhudumu mmoja kwa kila chumba.
Shane
O’Hare, Makamu Rais wa Masoko wa Shirika la ndege la Etihad alisema:
“Tunafurahishwa na uamuzi wa jopo la wataalamu wa tuzo za Globe Travel,
ambao ndio walipiga kura ‘Makazi’ kuwa huduma bora iliyovumbuliwa katika
sekta yetu. Vyumba hivi vimebadili mitazamo ya wengi, vikiwapa fursa
watu wa kawaida kufurahia huduma zinazopatikana mara nyingi katika ndege
binafsi tu.”
“Etihad
inathamini ushirikiano kati yake na soko la Uingereza, uhusiano
ulioanza tulipozindua safari zetu kuelekea na kutoka uwanja wa ndege wa
Heathrow uliopo jijini London mnamo mwaka 2004. Tumeinua hadhi ya
usafiri ikiwa ni pamoja na kuzipa ndege zetu muonekano halisia wa makazi
ya kuishi na kuwapa wasafiri viwango vya hali ya juu vya faragha na
utulivu”.
Huduma
ya ‘Makazi’ inapatikana ndani ya ndege aina ya A380 zinazofanya safari
zake kati ya Abu Dhabi na London, New York pamoja na Sydney. SHirika la
Etihad linatazamia kuzindua huduma hii katika ndege ziendazo Mumbai na
Melbourne mwaka huu.
Etihad
ina timu maalumu ambayo kazi yake pekee ni kuhakikisha wanaochagua
kusafiri na ndege zao wanaweza kufuruahia vyumba ya ‘Makazi’ wapendavyo.
Timu hii pia ipo karibu na watoa huduma maalum waliopo kwenye vyumba
hivi. Wateja wanapewa fursa ya kufurahia huduma mbalimbali wakiwa
wanasafiri na ndege hii ya Etihad zikiwemo; kuweka oda ya mahala pa
kula, burudani ndani ya ndege, matukio maalum kama sherehe za kuzaliwa,
maelezo kuhusu waendako na kadhalika. Watuapo, timu hiyo maalum (VIP)
huwasaidia wageni katika kufanya taratibu za kuwasili na usalama.
Ndege
za Etihad zinafanya safari zake kwenda Uingereza kutwa mara sita, pamoja
na kutoa huduma za safari za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa
Heathrow uliopo jijini London na kuelekea Machester na Ediburgh,
zilizoanzishwa Juni 8 mwaka jana. Uwanja wa ndege wa Heathrow ulipewa
nafasi kuwa kiwanja cha kwanza ndege aina ya Airbus A380 za Etihad kutua
kwa mara ya kwanza, na hivyo huduma hiyo ilianza mwishoni mwa mwaka
2014.