MY ADVERT EA SHOWBIZ

MY ADVERT EA SHOWBIZ

SIX OFFICE SOLUTION

MOCHRISPO

DARDY FASHION

Jan 18, 2016

WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UUZAJI WA MADAWA YA KULEVYA.

Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi (DCP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  ya Dar esSalaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo) Katika ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na watuhumia wa wizi na Madawa ya kulevya hapa nchini.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi (DCP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  ya Dar esSalaam, Simon Sirro akionyesha magari yenye namba za usajili T593 DEL aina ya Prado na jingine lenye namba T 999 DDB nalo Prado.
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam yawafikisha mahakamani watuhumiwa wawili wanaotuhumiwa kwa uuzaji wa madawa ya kulevya hapa nchini na biashara haramu ya binadamu.

Watuhumiwa hao ni Mohamed Abdalla Omari miaka 37 mfanyabiashara na mkazi wa Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, anatuhumiwa kwa kusafirisha madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu anatuhumiwa kwa kumsafirisha Mwinyi Mgobanya na kumweka rehani (Bond) huko Pakistani kisha kuchukua madawa ya kulevya kwa mali kauli na Nassoro Suleiman miaka 35 Meneja wa Tungwe Bureau De Change katika jengo la IPS jijini Dar es Salaam, anayetuhumiwa kwa kusa la kushiriki katika genge la wauza madawa ya kulevya na kusafirisha kiasi kikubwa cha pesa kwa njia ambazo si rasmi.

Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi (DCP), Kamanda wa Polisi Kanda Maalum  ya Dar es Salaam, Simon Sirro
 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo.

Pia Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam wamekamata magari na Pikipiki 24,068 na kutoza faini ya shilingi 722,040,000 katika Operesheni ya kukamata madereva wa magari na Pikipiki wanaovunja sheria za usalama barabarani, ikiwa  J
eshi  hilo halina lengo la kukusanya kiasi kikubwa cha fedha bali kuona watanzania wanatii sheria za usalama barabarani wakati wote wanapokuwa na vyombo vya moto.

Aidha Jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata waharifu sugu sita  kwa unyang'anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali na walipohojiwa walikiri kufanya uharifu huo kwa kutumia siraha.
 

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.