Hii ni barabara inayotegemewa na
daladala za Bwiru-Kisesa, Airtport- Kishiri pamoja na Ilemela-Kishiri
hii ikiwa ni kwa upande wa daladala. Lakini pia ikitegemewa na watumiaji
wengine wa vyombo vya moto vya binafsi.
Ni barabara iliyotumika pia na wakazi
wengi wa Jiji la Mwanza wakiwa wanatoka katika mizunguko yako ikiwemo
kutoka Soko Kuu la Jiji la Mwanza. Kama inavyoonekana katika picha
inahitaji msaada maana wakati huu wa mvua imeharibika sana.
"Hii barabara inaharibika mara kwa mara
kutokana na mitaro iliyopo hapa kuziba mara kwa mara kutokana na
wafanyabiashara katika maeneo haya kuwa na tabia ya kutupa makopo
mitaroni na hivyo kusababisha mitaro kuziba na hivyo mvua ikinyesha maji
yanajaa katika barabara hii na hatimae kusababisha hali hii unayoiona".
Binagi Media Group imeeleezwa na baadhi ya wafanyabiashara waliopo
jirani na barabara hiyo.
Watumiaji wa barabara hiyo wameiomba
halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana
kushughulikia ukarabati wa barabara hiyo pamoja na kusimamia suala la
usafi ili kuzuia uchafu kutupwa katika mitaro iliyo katika barabara hiyo
ili kuzuia kuziba na hatimae kusababisha uharibifu katika barabara
hiyo.
chanzo: BINAGI MEDIA