Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia), akimsikiliza Rais wa
Mahakama ya Afrika Jaji Mstaafu, Mhe. Augustino Ramadhani alipofika
kumtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa
Waziri. Pia kuzungumzia masuala mbalimbali yanayoihusu Mahakama hiyo
likiwemo suala la ujenzi wa Mahakama hiyo katika Jiji la Arusha.
Afisa
Mambo ya Nje, Bw. Elisha Suku naye akielezea jambo katika mazungumzo
kati ya Waziri Dkt. Mahiga na Mhe. Ramadhani (hawapo pichani), wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Baraka
Luvanda, na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizarani, Bi. Mindi Kasiga.
Mazungumzo yakiendelea.
Picha na Reginald Philip.