Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza na Waandishi wa Habari
kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Nyerere baada ya kuwasili akitoka
Songea Januari 6, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Geoge Simbachawene. na kulia ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es slaam Meck Sadiki.
Baadhi ya
waandishi wa habari wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere baada ya kuwasili akitoka
Songea Januari 6, 2016. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(PIcha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango
vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji
wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).
Akizungumza leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar
es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu
amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo
kasi. Ambapo nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi
Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi
1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli.
Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na
watumishi, mradi ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi
nje ya jiji, “Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi
na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu.
Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene na Waziri wa
Ujenzi , Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya
viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi huo.
Tarehe 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu
Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi
Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu
ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari
2016, imebainika kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala
kuanisha gharama za uendeshaji.